KIUTSO kuadhimisha siku ya ukimwi duniani kwa vipimo, ushauri na nasaa

Serikali ya Wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa Kampala nchini Tanzania (KIUTSO) 2022-2023 chini ya Wizara ya Afya na Jinsia Chuoni kwa kushiriakiana na “MY CHARITY ORGANIZATION” pamoja na Tanzania Medical Students’ Association (TAMSA) ilifanikisha zoezi la uchangiaji damu, vipimo vya ukimwi pamoja na vipimo vya afya ya kinywa na meno ambayo ilifanyika hapa chuoni jana tarehe 1 Desemba ambayo pia ilikua ni siku ya UKIMWI Duniani (World Aids Day).

Watoa huduma wa vipimo vya ukimwi na afya ya kinywa na meno walikua ni KBD Medical Specialized Polyclinic na zoezi la uchangiaji damu walikua ni wahudumu kutoka mpango wa taifa wa Damu salama kanda ya Mashariki.

Pia, tulipata bahati ya kutembelewa na Miss Tanzania 2022, Halima Kopwe ambaye ameshiriki zoezi la kuchangia damu pamoja nasi.

“Kiujumla zoezi zima limeenda vizuri sana tunawapongeza wote walioitikia wito wa kushiriki kikamilifu zoezi la siku ya leo watu wamechangia damu lakini pia wamefanya checkup ya afya zao ikiwemo Afya ya kinywa na meno, Uzito na urefu (BMI).” Alisema Raisi wa KIUTSO, Henry Katonge.

“Sambamba na hilo, wanafunzi wamepata elimu kuhusiana na homa ya ini, namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi na namna ya kusafisha na kutunza kinywa kwa ujumla,” Aliongezea Bwana Katonge.

“Salamu za pongezi kwa manajementi wote wakiongozwa na Makamu mkuu wa chuo kwa ushirikiano
wao kufanikisha zoezi la siku hii muhimu siku ya UKIMWI duniani,” ashukuru Makamu Raisi wa KIUTSO.

Takwimu za zoezi ya jana ilikua kama ifuatavyo:
Waliopima HIV- 90
Waliochangia damu-41
Afya ya kinywa na meno-101

Tangu mwaka 1988, siku ya kwanza ya mwezi wa Disemba imeteuliwa kuwa Siku ya UKIMWI Duniani, siku ya kimataifa inayojitolea kuhamasisha watu kuhusu janga la UKIMWI linalosababishwa na kuenea kwa maambukizi ya VVU na kuwakumbuka waliofariki kutokana na ugonjwa huo. Ugonjwa wa Upungufu wa Kinga Mwilini.

related

Search
Generic filters
Exact matches only

Having Trouble Applying? (je, unahitaji msaada wa kufanya maombi?)

Please fill in your details and one of our agents will contact you shortly.
(Tafadhali jaza hii fomu, moja wa wakala wetu atawasiliana nawe hivi punde)

NOTE : * Means Required (Lazima Ijazwe)

SiteLock