Mzee Mwinyi aanika mafanikio makubwa Serikali awamu ya sita

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania (KIUT), Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake ya awamu ya sita, kuchukua hatua za kuimarisha masuala ya Maendeleo nchini hususan katika elimu, jamii, na uchumi.

Rais mstaafu Mwinyi, alisema hayo jana katika mahafali ya tano ya chou cha KIUT, ambapo aliwatunuku wahitimu 669 vyetu vya Astashahada, Stashahada, na Shahada.

“Kupitia jukwaa hili, pia ninawaomba nyote muungane nami kuipongeza Serikali ya Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha taifa letu linazidi kuimarika kielimu, kijamii na kiuchumi.”

“Kupitia kaulimbiu yake ya kazi iendelee Rais Dk. Samia ametukumbusha kwa maneno na matendo kwamba; kazi ndio msingi wa Maendeleo na hakuna haki bila wajibu,” alisema.

Rais mstaafu Mwinyi aliwataka Watanzania na wanajumuiya wa chou hicho kwa ujumla kumuunga mkono Rais Samia, katika kujenga taifa la kistaarabu kupitia elimu bora.

Aliwahimiza kumuombea Rais Dk. Samia apate afya njema, aendelea kuitumikia nchi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

Aliwataka wahitimu hao kuyatumia maarifa vyema waliyopata chuoni hapo kwa manufaa ya taifa, kwa kuwa kasi ya Maendeleo katika uchumi hutegemea uwekezaji wa maarifa na ujuzi wa watu wake.

“Lakini uthibitisho mkubwa wa maarifa na ujuzi wenu utatokana na utendaji wenu huku muendako, kila mara katika utendaji wenu kumbukeni semi zilizojenga Tanzania; kuwa binadamu wote ni sawa,” alisema.

Professor Mgaya

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Profesa Yunus Mgaya, alisema Rais Dk. Samia kupitia serkali yake ya awamu ya sita amekisaidia chou hicho kuwa miongoni mwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu nchini.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Angwara Kiwara, alimshukuru Rais Dk. Samia kwa uongozi wake thabiti na kuboresha mazingira ya uwekezaji, ambao umeongeza imani ya bodi ya wadhamini kuwa salama.

Chanzo:
Gazeti ya Mzalendo tarehe 18 – 24 Desemba, 2022

Mwandishi:
Simon Nyalobi

related

Search
Generic filters
Exact matches only

Having Trouble Applying? (je, unahitaji msaada wa kufanya maombi?)

Please fill in your details and one of our agents will contact you shortly.
(Tafadhali jaza hii fomu, moja wa wakala wetu atawasiliana nawe hivi punde)

NOTE : * Means Required (Lazima Ijazwe)

SiteLock