Ili Taifa liwe na wataalamu wa afya wa kutosha, Watanzania hususani vijana wametakiwa kuchangamkia fursa za masomo zinazotolewa na Chuo cha Kimataifa cha Kampala nchini Uganda (KIU).
Hayo yamesemwa na Katibu wa Chuo hicho, Tawi la Dar es Salaam, Tanzania, Atukwatse, Judith wakati akizungumza na Upendo Media kuhusu mipango ya chuo hicho na kusema Watanzania wanaosoma kozi za afya wanapatiwa punguzo la Ada kutokana na upekee wa sekta hiyo.
Aidha wanafunzi wanaweza kuchagua kwenda kusoma nchini Uganda kwa gharama hizohizo zinatozwa KIU Tanzania kwa baadhi ya masomo ya afya,pia chuo kina hosteli kwa wanafunzi wanaotoka nje ya Tanzania.
Alisema fursa nyingine katika chuo hicho ni pamoja na Maabara za kisasa na Wanafunzi kufanya mazoezi kwa vitendo katika Hosptali za Chuo.
Mkuu wa Idara ya Elimu wa Chuo hicho cha Dar es Salaam, Tanzania, Dk. Thadei Mwereka alisema katika kuhakikisha wanafunzi wanaosoma hicho wanaiva vizuri na wana miundombinu  mizuri,maabara na vifaa vya kisasa vya kufundishia.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho ,Kemilembe Kamara na Shaffy Muriro walisema wanafundishwa namna ya kwenda kujiajiri na kusaidia kukabiliana na changamoto katika jamii.
Aidha waliongeza kuwa mazingira ya chuo ni rafiki ikilinganishwa na vyuo vingine,kutokana na kuwa na maeneo mengi ya kujisomea bila usumbufu pamoja na kuwa walimu wenye uzoefu mkubwa.
Aidha wanafunzi wanaweza kuchagua kwenda kusoma nchini Uganda kwa gharama hizohizo,pia chuo kina hosteli kwa wanafunzi wanaotoka nje ya Tanzania.
Chanzo:GAZETI la Upendo Media, tarehe 5 – 11/Machi/2023
Mwandishi: Vicent Kasambala