Mnamo tarehe 7 Machi, 2025 Wizara ya Afya kupitia mifumo yake ya ukusanyaji wataarifa na ufuatiliaji wa magonjwa ilipokea taarifa za uwepo wa wahisiwa wenye dalili za vipele usoni, mikononi, miguuni na sehemu nyingine za mwili. Dalili hizi ziliambatana na homa, maumivu ya kichwa, vidonda kooni, maumivu ya viungo vya mwili ikiwemo misulina mgongo. Kati ya wahisiwa hao mmoja ni dereva wa magari ya mizigo aliyetoka nchi jirani kwenda Dar es Salaam.
Baada ya kupokea taarifa za wahisiwa, sampuli zilichukuliwa na kupelekwa maabara ya Taifa kwa uchunguzi. Mnamo tarehe 9 Machi, 2025 uchunguzi wa kimaabara umethibitisha kuwa wahisiwa wawili (2) wana maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Mpox. Hivyo, hadi kufikia sasa jumla ya wahisiwa wawili (2) wamethibitika kuwa na ugonjwa wa Mpox nchini.
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na vituo vyote vya kutolea huduma za Afya, inaendelea na ufuatiliaji, uchunguzi na utambuzi kubaini kama kuna wahisiwa wengine ili waweze kupatiwa huduma stahiki.
Chanzo cha ugonjwa huu ni wanyama jamii ya nyani, ambapo binadamu huweza kuupata kutokana na shughuli zinazoweza kusababisha kugusana na wanyama, majimaji au nyama za wanyama wenye maambukizi. Aidha, endapo binadamu akipata maambukizi hayo anaweza kumwambukiza mtu mwingine kwa kugusana moja kwa moja.
Kwa taarifa hii, Wizara ya Afya, inawahakikishia wananchi kuwa Serikali imejipanga kudhibiti ugonjwa huu na hasa kutokana na uzoefu tulionao wa kudhibiti magonjwa ya mlipuko. Serikali inaendelea kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa katika ngazi zote, upimaji wa watu wanaoingia na kutoka kupitia mipaka ya nchi, kuimarisha utoaji wa elimu ya afya na kuhamasisha jamii ili kuwawezesha wananchi kuchuka hatua za kujikinga.
Kwa kuzingatia kuwa magonjwa mengi yanayosababishwa na virusi hayana tibamahususi ila mgonjwa anahudumiwa kulingana na dalili alizonazo. Hivyo Wizarainawasihinakuwasisitizawananchiwotekuzingatianakutekelezaafuazakujikinga kama ifuatavyo:
- Kuwahikatikakituochahudumazaafyakwauchunguzinamatibabuunapoona mojawapo ya dalili za ugonjwa wa Mpox au piga simu nambari 199 bila malipo;
- Kuepukakuchangiavitukamanguonamatandikoambavyovimetumiwanamtu mwenye dalili za Mpox;
- Kuepuka kugusana kwa kupeana mikono, kubusiana, kukumbatiana au kujamiiana na mtu mwenye dalili za Mpox;
- Kuepukakugusamajimajiyamwiliyamtumwenyedaliliza
- KuepukakumuhudumiamgonjwamwenyedalilizaugonjwawaMpoxbila kuchukua taharadhari;
- Watumishiwaafyakuzingatiakanunizakujikinganamagonjwawakatiwote wanapowahudumia wagonjwa ikiwemo wenye dalili za vipele na homa;
- Kunawamikonomarakwamarakwamajitiririkanasabuniaukutumiavitakasa
Wizara ya Afya, itaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa ugonjwa huu, kadri taarifa za ufuatiliaji na uchunguzi zitakavyopatikana. Wizara inashauri wananchi kuendelea na shughuli za kila siku kwa kuzingatia tahadhari za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu.
Vilevile, Wizara inapenda kuwapa taarifa kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa Marburg, ikumbukwe kwamba, mnamo tarehe 20 Januari 2025, Serikali ilihabarisha umma hukusu kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Marburg. Mwenendo wa udhibiti wa ugonjwa huu unaendelea vizuri na hadi kufikia leo tarehe 10 Machi 2025, zimetimia siku 41 bila kuwa na mgonjwa mpya.
Chanzo
JENISTAJ.MHAGAMA(MB)
WAZIRIWAAFYA – TANZANIA
TAREHE 10 MACHI, 2025, DODOMA
TOVUTI: https://moh.go.tz/storage/app/uploads/public/67c/efe/b3e/67cefeb3e7e94186575583.pdf