“Baadaye mwaka 2021 timu ya soka ya KIUT tulikwenda kuisajili Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na baadaye Chama cha Soka Ilala (IDFA), hivyo klabu yetu tukaruhusiwa kushiriki mashindano mbalimbali na tuna mpango kazi mzuri wa kufikia malengo yetu,” alisema.
Na SIMON NYALOBI
‘’KUPITIA Goli la Mama, kwa kusema ukweli Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ameleta chachu ya kufanya vizuri kwetu sisi wanamichezo na amefanya jambo jema kwa kuwa anatengeneza ajira nyingi kwa vijana.
“Rais Dk. Samia, ameiona sekta ya michezo ni miongoni mwa sekta zinazotoa ajira kwa wingi nchini, namwomba aendelee na hamasa hiyo, michezo yetu ipige hatua
kubwa.
Hayo ni baadhi ya maneno ya kocha wa timu ya soka ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIUT), tawi la Gongo la Mboto, Ilala, jijini Dar es Salaam, inayoshiriki michuano ya Ligi Daraja la Tatu, Wilaya Ilala, Erius Marius, alipofanya mahojiano na gazeti hili.
Marius alisema katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dk. Samia, kumekuwa na hamasa kubwa kupitia utaratibu wa kutoa zawadi ya fedha kwa timu zinazofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.
Alieleza katika miaka minne ya uongozi wa Rais Dk. Samia, utaratibu huo umempaisha na kuwapa changamoto wanamichezo kufanya vizuri.
Pamoja na hayo, alishauri serikali kuendelea kujenga na kuviboresha viwanja vya michezo vitakavyoleta hamasa ya vijana wengi kushiriki michezo.
Pia, kusaidia uwepo wa vifaa vya michezo kuanzia mipira, jezi na vitakavyorahisisha ushiriki wa wanamichezo katika michuoni mbalimbali.
Akizungumzia malengo ya timu hiyo, alisema ni kuhakikisha inapanda Ligi Kuu Tanzania Bara na kuendeleza vipaji vya wachezaji katika hatua mbalimbali.
 Alisema azimio la kufanya hivyo, lilifikiwa na uongozi wa timu hiyo kwa kushirikiana na uongozi chuo. hicho miaka mitano iliyopita.
“Mwaka 2020 KIUT ilichukua wazo la kuhamasisha michezo kuanzia soka na mingine, tukaona tusajili klabu katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT), ikiwa ni klabu ya michezo na mashindano.
“Baadaye mwaka 2021 timu ya soka ya KIUT tulikwenda kuisaj Shinkisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na baadaye Chama cha Soka Ilala (IDFA), hivyo klabu yetu tukaruhusiwa kushiriki mashindano mbalimbali na tuna mpango kazi mzuri wa kufikia malengo yetu,” alisema.
Alisema hivi sasa timu hiyo iko Ligi Daraja la Tatu, Wilaya ya Ilala inayosimamiwa na IDFA ambayo inatarajiwa kuanza mwezi huu katika viwanja mbalimbali.
Pia amesema imekuwa ikishiriki katika mashindano ya Ilala Samia Super Cup, ambayo hivi sasa yamefikia hatua ya timu 32 bora zikigawanywa katika makundi manne.
Aliweka wazi, mashindano ya Ilala Samia Super Cup,yamewaletea hamasa ya ushindani kwa kuwa yalishirikisha timu 100 yakiwa katika kanda nane.
‘Hadi tumefika hatua hii kazi imefanyika kweli kutoka timu 100 hadi kubakia timu 32, tumepambana na tunaamini tutachukua kombe hili’alisema.
Alieleza katika mashindano hayo wako katika kundi H, wakiwa na timu za Vingunguti Academy,Sinai Kombaini na Kerem FC.
Kama hiyo haitoshi, alisema timu hiyo imefanikiwa kushiriki mashindano mbalimbali,yakiwemo Ndondo Cup mwaka 2022 na kufika hatua ya finaili.
Alisema mwaka 2023, katika mashindano ya Ndondo Cup, walifika hatua ya 16 bora,vivyo hivyo mwaka huo ilishiriki katika mashindano ya Chama cha Famasia Tanzania [PST] na ligi ya Vijana ya Afrika Mashariki yaliyoandaliwa na SAFINA mwaka 2023.
Vivyo hivyo, wamekuwa wakishiriki katika mashindano ya Vyuo Vikuu Tanzania [TUSA], ambapo alisema maandalizi mwaka huu yanayatarajiwa kuanza Aprili katika Chuo cha Kilimo Sokoine(SUA), mkoani Morogoro
Akizungumzia mafanikio ya timu hiyo katika kuzalisha vipaji vya wachezaji vinavyotumika katika timu nyingine, hivi sasa aliwataja wachezaji hao na majina ya timu zao walizopo hivi sasa katika mabano ni Jesse Koti (KMKM ya Zanzibar) Hassan Hassan ( African Lyon), MathiasMarius(Malimao) na wengineo.
Alisema dhamira yao ni kuona wachezaji wengi kutoka katika timu hiyo wanasajiliwa na timu kubwa kutokana na mafunzo wanayowapa.
Marius ambaye alikuwa mchezaji wa timu hiyo hapo awali alisema alipofikia hatua ya kustaafu soka aliamua kuchukua kozi za ukocha katika ngazi mbalimbali, ndipo uongozi wa chuo ulipoamua kumpa mikoba ya timu hiyo.
“Nilijua nakwenda kustaafu soka, sasa nikaona nianze taratibu kujiingiza katika masuala ya menejimenti,kwa hiyo mwaka 2021 nilisoma kozi ya awali ya soka na baadaye nilisoma kozi ya Stashahada D,kozi zote zilisimamiwa na IDFA,alisema.
Alisema mwaka 2022, alipewa mikoba ya kuifundisha timu hiyo, baada ya makocha watangulizi wa timu hiyo mmoja kufariki dunia na mwingine kupata kibarua kwingine.Â
Aliweka wazi baada ya kupewa mikoba ya kufundisha timu hiyo, haikumpa shida kutokana na kufahamu misingi ya timu hiyo kinagaubaga.
Kocha huyo, alisema alianza kuiandaa timu hiyo na kucheza mechi za mitaani andazo ziliwapa uzoefu wa kwenda kucheza mashindano mbalimbali.
Kuhusu usajili wa wachezaji wa timu hiyo, alisema huwasajili wachezaji wa ndani ya chuo na nje ya chuo katika kuleta muunganiko mzuri wa timu.Â
Alisema uongozi wa chuo umekuwa ukitoa ufadhili wa masomo. kwa wachezaji wanaotaka kujiendeleza kimasomo.
Vivyo hivyo, alisema uongozi wa KIUT, hujishughulisha na jukumu la kuwalipa posho na gharama za timu kuanzia katika mazoezi na mashindano.
Kocha huyo alisema kutokana na huduma hizo kutoka uongozi wa chuo, wachezaji wamekuwa wakitulia na kutekeleza majukumu yao uwanjani.
CHANZO:Â
MWANDISHI: SIMON NYALOBI
CHOMBO CHA HABARI: GAZETI LA UHURU
TAREHE: 7 APRILI 2025 – JUMATATU