Mageuzi ya kihistoria katika miaka minne ya Rais Samia

Mhadhiri Msaidizi wa Uchumi wa Chuo kikuu cha kimataifa cha Kampala (KIUT), Tawi la Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam, Erius Marius, alisema Rais Dk. Samia, amechochea ukuaji wa Uchumi kutokana na miradi iliyopo nchini.

Marius, alisema ujenzi wa Barabara za mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART), Katika mkoa wa Dar es Salaam, hususani kutoka Gongo la Mboto hadi Kariakoo, yamechochea shughuli za Uchumi.

“Sasa hivi kuna ujenzi wa Barabara za Mabasi ya DART unaokwenda vizuri, umepiga hatua kubwa

“Nadhani ni asilimia 50 hado 60, katika Barabara ya Nyerere, watu wengi hawakutarajia iwapo mabasi haya yangekuja Gongo la Mboto, kwa muda mfupi, labda walidhani miaka 20 inayokuja,”alisema. 

Alisema wananchi hususani wa Gongo la Mboto, hivi sasa kabla ya kuanza usafari huo, wameanza kunufaika na biashara ya bidhaa mbalimabali kwa mafundi wanaojenga na wananchi waliopo karibu na maeneo Jirani.

“Wananchi wanauza chakula kwa mafundi wa ujenzi wa Barabara hiyo, wanauza na bidhaa nyingine na ukiangalia kumechangamka kwa shughuli za Uchumi hadi nyakati za usiku watu wanakimbizana katika biashara, lakini chanzo ni mradi ulioletwa na Rais Dk. Samia,” alisema.

Alisema mustakabali wa Uchumi wa eneo hilo baada ya kukamilika na kuanza kwa safari za mabasi hayo kunaashiria ukuaji wa Uchumi kwa wananchi na mapato ya serikali.

Pia, alisema ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami, katika maeneo pembezoni mwa miji hapa nchini imeleta chachu kwa wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali.

Akizungumzia usafiri wa treni inayotumia Reli ya kisasa(SGR), kutoka Dar es Salaam Kwenda Morogoro hadi Dodoma alisema kukamilika kwake kumeongeza chachu ya kufanya biashara katika mikoa hiyo.

Alisema wafanyabiashara kutoka katika mikoa hiyo wamekuwa wakitumia treni hiyo katika shughuli zao, hivo kuwa sehemu ya kichocheo cha Uchumi.

Pia alisema miradi iliyoanzishwa na serikali yake imekuwa ni Daraja la kukuza Uchumi katika maeneo mengine ikiwemo elimu bila malipo kuanzia shule za msingi hadi sekondari.

Alifafanua elimu bila malipo imechangia kuwapa wanafunzi uwezo wa maarifa ya uzalishaji wa bidhaa kitaalamu pindi wanapohitimu elimu zao.

“Ukitaka kuwa na Uchumi imara ni lazima watu wako uwape fursa ya elimu, hicho ndicho anachokifanya Rais Dk. Samia hivi sasa wananchi wake wanapata elimu baadaye wanakuwa wajuzi katika uzalishaji malighafi,” alisema.

Alisema msisitizo wa uliowekwa na serikali katika uzalishaji wa bidhaa bora katika viwanda vya ndani, kumeendelea kuondoa utegemezi wa kuagiza baadhi ya bidhaa kutoka nje ya nchi.

Katika afya, alisema amejitahidi kuhakikisha afya za watanzania zinakuwa bora, hivyo kujenga kwake zahanati na vituo vy afya vingi nchini kumelenga kuwanjengea afya bora wananchi washiriki katika shughuli za kuzalisha mali.

“Mfanyakazi hawezi kuzalisha bidhaa bora akiwa katika kiwanda au kampuni bila ya kuwa na afya bora na afya ni mtaji, kwa hiyo Rais Dk. Samia, kushughulikia suala la afya anawafanya Watanzania wawe na uwezo wa kuzalisha zaidi,” alisema

Mhadhiri huyo alisema katika kipindi hicho cha miaka minne, amedhihirisha kuwa, nchi imepata rais mpambanaji na mfatiliaji wa rasilimali za nchi na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

Aidha, alisema amekuwa mstari wa mbele katika kutafuta amani katika migogoro inayotokea katika nchi Jirani akitolea mfano mgogoro  wa Mashariki wan chi ya kidemokrasia ya Congo (DRC).

Alieleza katika kipindi hicho, amejitahidi kuimarisha umoja na mshikamano katika taifa licha ya watu wakitofautiana kwa itikadi zao.

Kwa jitihada hizo, alizofanya alimwomba iwapo atafanikiwa kushinda katika kiti cha Urais katika Uchaguzi mkuu wa mwaka huu, asisite kuendeleza alipoachia kwa kuwa, Watanzania wengi wanamuunga mkono.

Chanzo cha Habari

Mwandishi: Simon Nyalobi

Chambo cha Habari: Gazeti la Uhuru – Toleo Maalumu

related

Research Information Management

Research Projects

Having Trouble Applying? (je, unahitaji msaada wa kufanya maombi?)

Please fill in your details and one of our agents will contact you shortly.
(Tafadhali jaza hii fomu, moja wa wakala wetu atawasiliana nawe hivi punde)

NOTE : * Means Required (Lazima Ijazwe)

SiteLock