Na Victoria Godfrey.
Timu za MTC na Chuo Kikuu cha Kampala nchini Tanzania (KIUT) imeendelea kutoa dozi kwa wapinzani wao baada ya kuibuka na ushindi mfululizo katika michezo yao ya ligi ya wavu ya Muungano inayoendelea kutimua vumbi kwenye uwanja wa ndani wa Taifa Dar es salaam.
Nyota ya MTC, KIUT zilianza kung’ara baada ya kufanya vizuri katika michezo yake mfululizo,iliyochezwa jumatatu na jumanne ya wiki hii.
MTC ilianza kwa kupata ushindi wa seti 3-0 dhidi ya kigamboni huku michezo mwingine ilishinda seti 3-0 dhidi ya jeshi stars,huku KIUT ikicharaza jeshi stars kwa seti 3-2,huku mchezo wa pili ukitoka kidedea kwa seti 3-0 dhidi ya kigamboni.
Michezo mingine ya wanawake jeshi stars ilishinda seti 3-1 dhidi ya mkalapa ambao mchezo awali walipoteza dhidi ya JKT uliochezwa April 16 mwaka huu.
Mwenyekiti wa chama cha Mpira wa wavu Tanzania (TAVA) Jeneralu Mstaafu Patrick Mlowezi,alisema ligi inaendelea kwa ushindani mkubwa.
Chanzo: Zanzibar Leo ya Alhamisi tarehe 15 Aprili 2021