MTC yaongoza Wavu Muungano.

Timu ya MTC inaongoza katika msimamo wa ligi ya Muungano ya mpira wa wavu inayoendelea katika Uwanja wa Ndani wa Taifa,Dar es salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana,katibu Mkuu wa Chama Cha Mpira wa Wavu(TAVA),Fredy Selangia alisema ligi hiyo ilianza Aprili 12 na itamalizika kesho.

Ligi yetu inashirikisha timu 12, ambapo sita ni za wanaume na sita za wanawake, mpaka sasa MTC inaongoza ikiwa na pointi sita na jeshi stars na JKT za wanawake zina pointi sita kila mmoja,”alisema Selangia.

Alisema timu ya KIUT ya wanaume inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tano baada ya kucheza michezo miwili, JKT ina pointi tatu baada ya kucheza mchezo mmoja,Jeshi Stars ina Pointi moja baada ya kucheza michezo miwili na mafunzo na kigamboni hazina pointi.

Pia alisema Stars Girls ina pointi tatu ikiwa imecheza michezo miwili na Mkalapa,KIUT na Chui hazina Pointi.

related

Research Information Management

Research Projects

Having Trouble Applying? (je, unahitaji msaada wa kufanya maombi?)

Please fill in your details and one of our agents will contact you shortly.
(Tafadhali jaza hii fomu, moja wa wakala wetu atawasiliana nawe hivi punde)

NOTE : * Means Required (Lazima Ijazwe)

SiteLock