KIUTZ mabingwa Netiboli Dar es salaam

Timu ya Chuo Kikuu cha Kampala Tanzania (KIUTZ) imetawazwa kuwa mabingwa wa ligi ya netiboli Daraja la tatu mkoa wa Dar es salaam iliyomalizika jumatatu ya wiki hii kwenye uwanja wa chuo hicho.

Nafasi ya pili imechukuliwa na Ustawi Queens, wakati Upendo Queens ikikamata nafasi ya tatu wote wakiondoka na zawadi ya makombe.

Kwa washindi mmoja mmoja mchezaji bora ilichukuliwa na kurthum kutoka Kampala,huku nafasi ya mzuiaji bora ikienda kwa Winfrida Robert (ustawi Queens), wakati mfungaji bora ameibuka Faraja kutoka (Kampala) na nafasi ya MVP imechukuliwa na Sia Jackson (upendo Queens)

Akizungumza na Zanzibar leo kocha mkuu wa Kampala Amad Msabaha alisema mazoezi, kujituma na kufuata mafunzo waliojifunza ndio siri ya ushindi huo.

Alisema mipango na kuendelea na mazoezi ya nguvu ya kujiandaa na ligi daraja la pili ngazi ya Taifa ya msimu ujao.

Naye mwenyekiti wa chama cha Netiboli Mkoa wa Dar es salaam (CHANEDA) Winfrida Emmanuel, alizipongeza timu shiriki na zilizoshinda katika ligi hiyo na kuzitaka kwenda kujipanga vyema kwa ajili ya ligi Daraja la pili waweze kuonyesha ushindani.

Mwenyekiti alisema timu mbili zimepanda ndio zitakazowakilisha mkoa wa Dar es salaam katika ligi hiyo ambazo ni Kampala na ustawi Queens.

Kwa upande wake katibu Mkuu wa chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) Judith Illunda, alikipongeza chama kwa kumaliza ligi yao na kuitaka mikoa mingine kuiga mfano huo ili kupata wawakilishi wa ligi daraja la pili ngazi Taifa.

NA VICTORIA GODFREY (Zanzibar Leo)

related

Research Information Management

Research Projects

Having Trouble Applying? (je, unahitaji msaada wa kufanya maombi?)

Please fill in your details and one of our agents will contact you shortly.
(Tafadhali jaza hii fomu, moja wa wakala wetu atawasiliana nawe hivi punde)

NOTE : * Means Required (Lazima Ijazwe)

SiteLock