NA VICTORIA GODFREY
Timu ya Kampala University, Kinondoni Utd zimeanza vyema katika michezo yao ya kwanza yah atua ya 32 bora, iliyochezwa jumatatu(juzi) kwenye viwanja tofauti, Dar es salaam.
Kampala iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Majohe UTD mchezo uliochezwa uwanja wa Bandari Temeke,Dar es salaam.
Dakika ya 33, 48 Kampala ilifunga mabao mawili yaliyofungwa na Thadei Ally, Juju Majohe UTD ilijipatia bao la kufutia machozi dakika ya 57 lililofungwa na Omary Ramadhan na Abdulrahman Bausi wa Kampala aliongeza bao la tatu dakika ya 90.
Wakati Kinondoni UTD ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya zofa FC mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa kinesi,Dar es salaam.
Mabao ya Kinondoni UTD yakifungwa dakika 40,66 ambalo la pili lilipatikana kwa njia ya penalti yaliyofungwa na Rashid Mchelenga.
Akizungumza na Zanzibar leo baada ya mchezo kumalizika kocha mkuu wa kampala inter joseph Marwa,alishukuru kwa kumaliza salama na kupata matokeo mazuri na kuvuna pointi tatu.
Alisema sasa mipango yao ni kuelekeza nguvu,akili na mawazo kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo ujao dhidi ya Kinondoni UTD utakaopigwa julai 21 mwaka huu dimba la kinesi, Dar es salaam.
Kwa upande wa kocha mkuu wa majohe UTD Abdallah Rashid,alisema wamekubali matokeo wamepoteza wapinzani wao walitumia udhaifu wao na kupata ushindi katika mchezo huo.
Source: Zanzibar Leo Date: 14th of July 2021