Tarehe 31 Mei 2025, Bunge lilimpa tuzo maalumu Rais Dk. Samia, ambapo Spika Dk. Tulia Ackson, alisema wabunge walitoa tuzo hiyo baada ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita kuakisi utawala bora, weledi, uwajibikaji, uaminifu na ujumuishi.
Baadhi ya wasomi walizungumza na kutoa maoni yao kwa Gazeti la Uhuru, akiwemo Bwana Erius Marius, ambaye ni Mhadhiri msaidizi wa Biashara na Uchumi wa Chuo cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania (KIUT), illiopo Gongo la Mboto, ilala, Dar es Salaam.
Bwana Erius Marius alisema Rais Dkt. Samia ameonesha uthubutu katika kuongoza nchi na kua amestahili kutunukiwa tuzo hiyo kutokana na kazi kubwa aliyoifanya katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.
Marius alisema uamuzi uliokuwa akifanya katika kipindi hicho, ulijikita katika busara akijali maslahi ya wananchi wake.
Akizungumzia uhusiano wa kimataifa, alisema Rais Dk. Samia ameboresha uhusiano wa kimataifa hatua iliyojidhirihisha kwenda katika nchi mbalimbali amabako kulisaidia ujenzi wa uchumi imara.
“Alipoingia madarakani aliahidi kudumisha ushirikiano wa kimataifa katika kujenga uchumi, aliamini bila ya hivyo nchi haiwezi kuuza au kununua bidhaa zake na hili aliweza, tukaona akishiriki na filamu ya Tanzania The Royal Tour,” alisema Marius.
Mhadhiri huyo alisema Rais Dk. Samia ameitangaza vyema sekta ya utalii ya Tanzania kupitia filamu hiyo.
Mbali na kuvutia watalii, alisema filamu hiyo imesaidia kuleta idadi kubwa ya wawekezaji na kupata misaada ya kimataifa katika kuendeleza baadhi ya miradi ya maendeleo.
Alieleza uongozi wake umeakisi dhana ya usawa wa kinjisia, kwa sababu jamii nchini na jumuiya za kimataifa, zimemshuhudia akiwa mwanamke aliyetekeleza majukumu yake vizuri.
Erius Marius – Hadhiri Msaidizi wa Biashara na Uchumi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania (KIUT)
“Amedhihirisha wanawake wakipewa uongozi wanaweza kwa maendeleo mengi amefanya na utendaji bora, hii imeondoa dhana iliyokuwepo mwanamke hawezi kufanya uamuzi mkubwa wowote,” alieleza Marius.
Chanzo:
Mwandishi: Simon Nyalobi
Chomba cha Habari: Gazeti la Uhuru
Tarehe: Jumatatu Juni 2, 2025