Muhtasari:
72 Pointi alizofunga KIUT dhidi ya 54 za DB Oratory na kuibuka mabingwa wa Provincal
KIUT imedhihirisha ubora wake baada ya kuifunga DB Oratory kwa point 72-54 katika fainali ya kombe la Provincal kwenye Uwanja wa Don-Bosco Osterbay.
Mashindano hayo ya Kombe la Provincal yaliandaliwa na kituo cha Don-BoscoOsterbay yakishilikisha DB VTC,Don Rua,IFM,Kigamboni Academy, DB Oratory,MUHAS na KIUT.
Katika mchezo huo KIUT ilidhibiti eneo lote la uwanja hali iliofanya DB kupoteana na kuchapwa katika robo zote nne kwa point 20-13,15-12,14-12 na 23-17.
Samson Mabula wa KIUT kwa kufunga pointi 28,huku akifunga tisa kwa mitupo ya pointi tatu na asisti saba akifuatiwa na Douglas Mollel aliefunga 19,huku Dominic Kipingu wa DB Oratory akifunga 12.
Kocha wa KIUT Denis Funganoti alipongeza timu zote kwa ushindani mkubwa walionyesha kwa siku zote.
“Timu zilipambana kwa kweli, na ushindi wetu ulichangiwa na maandalizi tuliokuwa tunafanya katika uwanja wa KIUT,” alisema Funganoti.
Alisema mashindano hayo pia ni moja ya maandalizi yao ya ligi ya kikapu Mkoa wa Dar es Salaam BDL mwaka huu na yanaenda vizuri.
Chanzo: Gazeti la Mwanaspoti ya Ijumaa, Februari 7, 2025.