na VICTORIA GODFREY
UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania [KIUT] umesema utaendela kuwekeza ili kupata wachezaji wazuri katika mchezo wa wavu waweze kwenda kushindana kimataifa.
Hivi karibuni timu ya chuo hicho kwa mchezo wa mpira wa wavu wanawake na wanaume imeshiriki mashindano ya kimataifa yaliyopewa jina KAVC yaliyo malizika nchini Uganda.
Akizungumza na zanzibarleo rais wa michezo wa KIUT Peter Kaahwa, alisema kuendelea kusaka vipaji kwa kuwawezesha kimichezo na elimu ya darasani.
Alisema lengo ni kuhakikisha wanaongeza nguvu katika kikosi kilichopo ili kiwe katika ushindani kwa mashindano ya ndani na nje ya Tanzania.
Naye meneja wa KIUT Mushabe Rogers, alisema wamejifunza ya nchi shiriki zilizofanya uwekezaji wa timu za vijana wadogo na kuwapa fursa ya kushiriki na kuleta ushindi.
”Kwa kweli ushiriki wetu kimataifa imewaongezeka wachezaji wetu kujipima viwango vyao na wachezaji wa nchi nyingine, kwetu ni fursa ya kujifunza wanafanya nini ili kushinda,” alisema Rogers.
CHANZO: ZANZIBAR LEO – GAZETI