UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala Tanzania [KIUT] umesema umejipanga kuonesha mapinduzi katika mashindano ya vyuo vikuu.
Mashindano hayo yamepangwa kufanyika kuanzia disemba 13 hadi 21 kwenye skuli ya sekondari Galanos jijini Tanga.
Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na yana simamiwa na shirikisho la michezo ya vyuo vikuu Tanzania [TUSA] yakishirikisha vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.
Akizungumza na Zanzibarleo raisi wa chuo hicho Peter Khawaa, alisema lengo ni kuhakikisha wanafanya vizur ili kuweza kujitangaza zaidi.
Alisema wachezaji wa michezo mbalimbali kujifua na kujiweka tayari kwa mashindano hayo.
Alisema KIUT watashiriki michezo ya netiboli wavu, kikapu wanawake Na wanaume, soka Na kabaddi ambao unaendelea kutambulishwa kwa vyuo vingine kwa mwaka huu.
Chanzo: VICTORIA GODFREY – Zanzibar Leo