OFISA Michezo wa Chuo cha Kampala University (KIUT), Martin Mbapila amesema ubingwa walioupata timu ya chuo hicho cha mashindano ya kikapu ya Vyuo Vikuu nchini (TUSA) mkoani Tanga umechangiwa na maandalizi mazuri waliyoyafanya mapema kabla ya kwenda kuchuana.
Mbapila aliliambia Mwanaspoti kwa simu muda mfupi baada ya timu hiyo kukishinda Chuo cha Ushirika Moshi (MoCo) kwa pointi 52 – 39 katika fainali, alisema maandalizi ya KIUT yalianza kabla ligi ya BD Division 1 kuanza na ndio maana yamewafanya watishe kwa kushinda michezo yot kwenye mashindano hayo yaliyofanyikia kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Mbapila alivitaja vyuo walivyovifunga ni: MUHAS, ARU, SAUT, MUCE, MoCo, na upande wa Zanzibar ilikua SUZU, ZU na SUMAIT.
“Kwakweli tulijipanda vizuri katika mashindano hay ana kikubwa zaidi kilichochewa ni uongozi wa chuo kuwa karibu na wachezaji wakiwatia moyo, hali iliyofanya wachezaji wabadilike kiuchezaji na kuwezesha timu kubebea ubingwa kibabe,” alisema Mbapila.
Mbapila alisema wanasahau mafanikio ya TUSA na sasa wanajipanga kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), aliyowahi kuishiriki akiwa na timu ya Chang’ombe Boyz miaka ya nyuma ya kutwaa tuzo kama Mchezaji Bora wa ufungaji wa maeneo ya mitupo ya point tatu (three pointer) na kudai anafikiria kurejea tena.
CHANZO: GAZETI LA MWANASPOTI