Timu za mambul,tegeta na Kiut zimeibuka mabingwa wa mashindano ya safina top 8 ya ligi ya vijana yaliyofanyika uwanja wa uhuru, Dar es salaam kuanzia Desemba 14,mwaka huu. Timu ya kituo cha mamboul kutoka Zanzibar iliifunga timu ya kituo cha IBG kwa bao 3-2 katika fainali ya vijana waliochini ya umri wa miaka 15.
Tegeta ilitanganzwa mabingwa kwenye fainali ya vijana waliochini ya umri wa miaka 17 kwa kuifunga timu ya kituo cha mwenge kwa bao 1-0 na timu ya kituo cha Chuo Kikuu cha Kampala(KIUT) U20 iliifunga timu ya kituo cha wachambuzi kwa mabao 3-2. Kwa ushindi huo kila timu iliondoka na kombe na medali za dhahabu na washindi wa pili walipata medali za fedha wakati mfungaji bora Masoud Machano kutoka mamboul alipata kombe.
Akizungumza wakati wa kufunga mashindano hayo ofisa michezo Tanzania (BMT),Charles Mazugu aliipongeza taasisi ya safina kwa kuendesha ligi za vijna. “nawapongeza waandaji wa mashindano haya na nimeambiwa na TFF (shirikisho la mpira wa miguu tanzania)wanayafahamu Na wachezaji wenye vipaji wanachaguliwa kwa ajili ya timu za taifa za umri mbalimbali ,”alisema maguzu.
Awali akimkaribisha mgeni ramsi,mkurugenzi kituo cha safina,Daniel Msangi alisema wameanzisha mashindano hayoo ili kuwapa wachezajii chipukizi nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.
Alisema jumla ya timu 24 zilishiriki mashindano hayo ambayo yalifungwa juzi.