KIUT Campus

Latest News

Stay updated with the latest news and events from Kampala International University in Tanzania.

Profesa Msolla aonya matumizi kupita kiasi ya AI kwa wanafunzi

AcademicDecember 5, 2025
Profesa Msolla aonya matumizi kupita kiasi ya AI kwa wanafunzi

Muktasari: Profesa Msolla ameonya matumizi ya AI kwa wanafunzi, akisisitiza ujuzi kuchochea maendeleo, huku KIUT kikitunuku wahitimu 1,484 katika ngazi mbalimbali za elimu.

Dar es Salaam. Mkuu wa Chuo cha Kimataifa cha Kampala Tanzania (KIUT), Profesa Peter Msolla ameonya matumizi kupita kiasi ya akili mnemba (AI) kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, akisema yanafifisha uwezo wao wa kufikiri.

Amesema kasi ya maendeleo ya uchumi hutegemea zaidi maarifa na ujuzi, hivyo ni muhimu wahitimu wa vyuo vikuu kutumia elimu waliyoipata kuchangia maendeleo ya nchi.

Aidha, amebainisha juhudi za Serikali kuboresha sekta ya elimu zimeongeza kasi ya mahitaji ya elimu ya juu na kuchochea uwekezaji katika chuo hicho.

Profesa Msolla ameyasema hayo leo Alhamisi Desemba 4, 2025 katika mahafali ya nane ya KIUT yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo zaidi ya wanafunzi 1,484 wametunukiwa ngazi mbalimbali za elimu.

"Tunaishi katika ulimwengu wa kidijitali tujihadhari na matumizi ya akili mnemba, siku hizi walimu wakitoa tu kazi mwanafunzi anakwenda anabonyeza anapata taarifa anayohitaji, hii linakwenda kufifisha ufikiri wanafunzi kwa hiyo kila kinachokuja kina hasara na faida zake.”

“Ni matumaini yangu kuwa ufaulu wenu ni ushahidi kuwa mmepata maarifa katika fani mlizosomea, jamii inataraji mna upeo wa hali ya juu katika kupambana na changamoto zinazokwamisha maendeleo, lakini uthibitisho utakuwa kwenye utendaji wenu huko mwendako," amesema.

Akizungumzia maboresho ya chuo hicho, Profesa Msolla amesema tayari wameweka mipango ya kukamilisha hospitali ya chuo hicho kufikia mwishoni mwa mwaka 2026.

Amesema hospitali hiyo itatoa huduma kwa jamii na kuwa kituo cha mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi.

"Baraza la chuo limedhamiria kuboresha miundombinu ya kujifunzia kama maabara, viwanja vya michezo pamoja na hosteli," amesema.

Kwa upande wake, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Honoratha Mushi, amesema chuo kimeboresha miundombinu ya kufundishia, maabara, vifaa vya kisasa na ubora wa rasilimali watu.

Pia amesema KIUT imejipanga kuongeza uwezo wa kudahili ili kuunga mkono juhudi za Serikali ambazo zimekuwa kubwa katika sekta ya elimu.

Profesa Mushi amesifu juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mazingira ya uwekezaji, ambayo yameipa uhakika bodi ya chuo kuendelea na uwekezaji.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Profesa Yunus Mgaya, amesema kuongoza chuo kikuu binafsi kinachotoa elimu ya sayansi na teknolojia si jambo dogo, kwani kunahitaji rasilimali watu, fedha na uongozi madhubuti unaofuata sera, sheria na kanuni za elimu ya juu.

"Uongozi wa chuo unaendelea kuonyesha weledi, maoni na uadilifu. Baraza la chuo limefarijika na mafanikio haya na linaamini uongozi bora utaendelea kuleta matunda zaidi," amesema.

Kati ya wahitimu 1,484 waliotunukiwa ngazi mbalimbali za elimu, 772 ni wanaume na 712 ni wanawake. Wenye vyeti vya stashahada ni 821, ambapo wanaume ni 381 na wanawake 440. Wenye shahada ya kwanza ni 641 na wenye shahada ya uzamili ni 22 pekee. Chanzo: Mwandishi: Baraka Loshilaa Chomba cha Habari: Gazeti la Mwananchi Tarehe: Alhamisi, Desemba 04, 2025 Tovuti:https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/profesa-msolla-aonya-matumizi-kupita-kiasi-ya-ai-kwa-wanafunzi-5286830

Stories You May Like

KIUT Workshop Inspires New Teaching Excellence

KIUT Workshop Inspires New Teaching Excellence

Nov 6, 2025

Parents urged to complete polio vaccinations for children

Parents urged to complete polio vaccinations for children

Oct 6, 2025

KIUT dominates TVNL, sweeps top individual awards

KIUT dominates TVNL, sweeps top individual awards

Sep 30, 2025

Wazazi wahimizwa kukamilisha chanjo ya polio kwa usalama wa watoto

Wazazi wahimizwa kukamilisha chanjo ya polio kwa usalama wa watoto

Aug 31, 2025

Mainland Netball League to kick off in Tabora on September 26

Mainland Netball League to kick off in Tabora on September 26

Aug 28, 2025

Tanzania volleyball team from Kampala international university shine at grand palace hotel international tournament

Tanzania volleyball team from Kampala international university shine at grand palace hotel international tournament

Aug 15, 2025

KIUT Prioritizes Athlete Health

KIUT Prioritizes Athlete Health

Aug 13, 2025

Tanzania Prisons, KIUT crowned TVNL Champions

Tanzania Prisons, KIUT crowned TVNL Champions

Sep 29, 2025

Boosting mental wellness across Tanzanian universities

Boosting mental wellness across Tanzanian universities

Oct 28, 2025

KIUT Joins Inaugural MAMODEX Malaria Modelling Meeting in Nairobi

KIUT Joins Inaugural MAMODEX Malaria Modelling Meeting in Nairobi

Dec 2, 2025

KIUT Shines at Zanzibar Exhibition

KIUT Shines at Zanzibar Exhibition

Aug 15, 2025

KIUT Volleyball Dominates 2025 TVF Awards After Landmark Season

KIUT Volleyball Dominates 2025 TVF Awards After Landmark Season

Dec 22, 2025

Art, Mindfulness, and Medicine

Art, Mindfulness, and Medicine

Jan 21, 2026

Kampala University Vice Chancellor warns excessive AI use undermines students’ critical thinking.

Kampala University Vice Chancellor warns excessive AI use undermines students’ critical thinking.

Dec 12, 2025

Breaking the Silence: TAMSA KIUT Takes on Female Genital Schistosomiasis

Breaking the Silence: TAMSA KIUT Takes on Female Genital Schistosomiasis

Jan 28, 2026

TAMSA KIUT & African Mothers Join Forces for Community Health

TAMSA KIUT & African Mothers Join Forces for Community Health

Jan 28, 2026

Building Hope: The KIUT Social Work Club Visits Fadhila Orphanage

Building Hope: The KIUT Social Work Club Visits Fadhila Orphanage

Jan 28, 2026

KIUT Debuts Building Youth Talk Initiative to Support Future Leaders

KIUT Debuts Building Youth Talk Initiative to Support Future Leaders

Jan 29, 2026

The KIUT-Halotel 5G Revolution

The KIUT-Halotel 5G Revolution

Feb 9, 2026

Checkmate in Dar Es Salaam: The Rafiki Tournament

Checkmate in Dar Es Salaam: The Rafiki Tournament

Feb 9, 2026

A 360-Degree Support Network: KIUT’s Proactive Stand Against GBV and Emotional Distress

A 360-Degree Support Network: KIUT’s Proactive Stand Against GBV and Emotional Distress

Feb 10, 2026

KIUT Social Work Association at the Temeke International Women’s Day Forum

KIUT Social Work Association at the Temeke International Women’s Day Forum

Mar 18, 2026

TMCS–KIUT Hosts Lenten Charity Outreach

TMCS–KIUT Hosts Lenten Charity Outreach

Mar 16, 2026

International Women’s Day 2026: KIUT Stands for Equality

International Women’s Day 2026: KIUT Stands for Equality

Mar 19, 2026

MAMODEX Advances to Operational Phase of Project

MAMODEX Advances to Operational Phase of Project

Mar 20, 2026