KIUT Campus

Latest News

Stay updated with the latest news and events from Kampala International University in Tanzania.

Wazazi wahimizwa kukamilisha chanjo ya polio kwa usalama wa watoto

ClubsAugust 31, 2025
Wazazi wahimizwa kukamilisha chanjo ya polio kwa usalama wa watoto

Muktasari: Wataalamu wamesema polio haina tiba na kutomaliza chanjo huongeza hatari ya madhara makubwa, ikiwamo kuharibika kwa mfumo wa neva na kupoteza uwezo wa kutembea. Dar es Salaam. Wazazi na walezi wamehimizwa kuzingatia umuhimu wa chanjo ya polio kwa watoto, ili kuwaepusha na madhara mbalimbali yakiwamo ulemavu wa kudumu. Wito huo umetolewa wakati wa kampeni ya uhamasishaji inayoendeshwa kwa ushirikiano kati ya Hospitali ya Mwananyamala na Rotary Club ya Mikocheni, ikilenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu athari za ugonjwa huo na umuhimu wa chanjo kama kinga madhubuti.  Kampeni hiyo ni i sehemu ya maandalizi kuelekea Siku ya Polio Duniani inayoadhimishwa Oktoba 24 kila mwaka.

Elimu hiyo inawalenga watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, ambao ndiyo waathirika wakuu wa maradhi hayo, yanayoweza kusababisha ulemavu wa kudumu kwa watoto. Akizungumza na kinamama hospitalini hapo Agosti 30, 2025, wakati wa utoaji wa elimu, mtaalamu wa masuala ya afya, Eunice Toonde, amesema wazazi wengi bado wanashindwa kutambua athari za ugonjwa wa polio, hivyo wapo wanaoshindwa kumaliza ratiba za chanjo kwa watoto wao.

"Ingawaje hatuna visa vingi vya ugonjwa wa polio hivi karibuni, sababu ya kutoa elimu ya umuhimu wa kumaliza chanjo ni kutaka kustawisha hali tuliyo nayo, kwani kutomaliza chanjo ya polio kwa watoto chini ya miaka mitano kunaweza kusababisha madhara mengi, yakiwemo ulemavu wa kudumu, kuharibika mfumo wa neva, kupoteza uwezo wa kutembea au kuwa na matatizo makubwa ya kudumu katika viungo vya mwili," amesema Eunice. "Polio inaweza pia kuathiri misuli ya kupumua, hali inayoweza kusababisha kifo kama mtoto hapati matibabu ya haraka," ameongeza.

Eunice amesisitiza kuwa polio haina tiba, bali kinga pekee ndiyo inayoweza kuzuia maambukizi, hivyo ni muhimu kutoa elimu kuhusu umuhimu wa chanjo ya ugonjwa huo kwa watoto.

Kwa upande wake, Catherine Moshi, mwanafunzi wa mwaka wa nne katika Chuo cha KIUT anayesomea udaktari, amesema wazazi wengi hawajui kinga za aina gani watoto wao wanapewa, na hivyo wanapowaona watoto hawana dalili yoyote, hawaoni umuhimu wa kumaliza chanjo ya polio, jambo linaloweza kuwa hatari kwa afya ya mtoto.

"Kinamama wanatakiwa kuhakikisha wanawapatia watoto wao na kumaliza chanjo ya polio. Mtoto hupokea chanjo ya polio wiki ya kwanza tangu kuzaliwa, na baada ya wiki sita, kumi na nne na kumi na sita, ili kumuepusha na polio," amesema Catherine.

Naye Rais wa Rotary Club Mikocheni, Nasibu Mahinya, amesema lengo la kutoa elimu hiyo katika Hospitali ya Mwananyamala ni kutokana na ufanisi mdogo wa kumfikia kila mjamzito na mlezi, hususan baada ya kugundua wengi hawafahamu madhara ya polio.

"Licha ya mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza ugonjwa wa polio, bado wapo kinamama wengi wasiojua madhara ya polio, hivyo tukaona ni muhimu kutoa elimu hii hadi kilele cha Siku ya Polio Duniani," amesema Mahinya.

Mahinya ameongeza kuwa kampeni za uhamasishaji zitakazofanyika kwa miezi michache ijayo, ili kuelimisha kinamama na walezi juu ya umuhimu wa kumaliza chanjo ya polio kwa watoto.

Muuguzi Mkufunzi kutoka Wizara ya Afya, Gloria Mwankenja, ametoa mfano wa mataifa kama Afghanistan na Pakistan, ambayo bado yanakumbwa na changamoto kubwa ya ugonjwa wa polio, na kusema kuwa muingiliano wa watu ni mojawapo ya sababu zinazofanya elimu hiyo kuwa muhimu zaidi.

"Kwa sasa, Tanzania imedhibiti ugonjwa wa polio, na mtoto wa mwisho kugundulika na ugonjwa huo alikuwa Mei 26, 2023 katika Manispaa ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa," amesema Gloria.

Elimu hiyo itaendelea kutolewa kwa wananchi hadi Oktoba 24, ambapo Siku ya Polio Duniani itakuwa ikiadhimishwa duniani kote, ikiwa na lengo la kutokomeza ugonjwa wa polio kabisa. Chanzo: Chomba cha Habari: Gazeti la Mwananchi Mwandishi: Mintanga Hunda Tarehe: Jumapili, Agosti 31, 2025

Stories You May Like

KIUT Workshop Inspires New Teaching Excellence

KIUT Workshop Inspires New Teaching Excellence

Nov 6, 2025

Parents urged to complete polio vaccinations for children

Parents urged to complete polio vaccinations for children

Oct 6, 2025

KIUT dominates TVNL, sweeps top individual awards

KIUT dominates TVNL, sweeps top individual awards

Sep 30, 2025

Mainland Netball League to kick off in Tabora on September 26

Mainland Netball League to kick off in Tabora on September 26

Aug 28, 2025

Tanzania volleyball team from Kampala international university shine at grand palace hotel international tournament

Tanzania volleyball team from Kampala international university shine at grand palace hotel international tournament

Aug 15, 2025

KIUT Prioritizes Athlete Health

KIUT Prioritizes Athlete Health

Aug 13, 2025

Tanzania Prisons, KIUT crowned TVNL Champions

Tanzania Prisons, KIUT crowned TVNL Champions

Sep 29, 2025

Boosting mental wellness across Tanzanian universities

Boosting mental wellness across Tanzanian universities

Oct 28, 2025

KIUT Joins Inaugural MAMODEX Malaria Modelling Meeting in Nairobi

KIUT Joins Inaugural MAMODEX Malaria Modelling Meeting in Nairobi

Dec 2, 2025

KIUT Shines at Zanzibar Exhibition

KIUT Shines at Zanzibar Exhibition

Aug 15, 2025

Profesa Msolla aonya matumizi kupita kiasi ya AI kwa wanafunzi

Profesa Msolla aonya matumizi kupita kiasi ya AI kwa wanafunzi

Dec 5, 2025

KIUT Volleyball Dominates 2025 TVF Awards After Landmark Season

KIUT Volleyball Dominates 2025 TVF Awards After Landmark Season

Dec 22, 2025

Art, Mindfulness, and Medicine

Art, Mindfulness, and Medicine

Jan 21, 2026

Kampala University Vice Chancellor warns excessive AI use undermines students’ critical thinking.

Kampala University Vice Chancellor warns excessive AI use undermines students’ critical thinking.

Dec 12, 2025

Breaking the Silence: TAMSA KIUT Takes on Female Genital Schistosomiasis

Breaking the Silence: TAMSA KIUT Takes on Female Genital Schistosomiasis

Jan 28, 2026

TAMSA KIUT & African Mothers Join Forces for Community Health

TAMSA KIUT & African Mothers Join Forces for Community Health

Jan 28, 2026

Building Hope: The KIUT Social Work Club Visits Fadhila Orphanage

Building Hope: The KIUT Social Work Club Visits Fadhila Orphanage

Jan 28, 2026

KIUT Debuts Building Youth Talk Initiative to Support Future Leaders

KIUT Debuts Building Youth Talk Initiative to Support Future Leaders

Jan 29, 2026

The KIUT-Halotel 5G Revolution

The KIUT-Halotel 5G Revolution

Feb 9, 2026

Checkmate in Dar Es Salaam: The Rafiki Tournament

Checkmate in Dar Es Salaam: The Rafiki Tournament

Feb 9, 2026

A 360-Degree Support Network: KIUT’s Proactive Stand Against GBV and Emotional Distress

A 360-Degree Support Network: KIUT’s Proactive Stand Against GBV and Emotional Distress

Feb 10, 2026

KIUT Social Work Association at the Temeke International Women’s Day Forum

KIUT Social Work Association at the Temeke International Women’s Day Forum

Mar 18, 2026

TMCS–KIUT Hosts Lenten Charity Outreach

TMCS–KIUT Hosts Lenten Charity Outreach

Mar 16, 2026

International Women’s Day 2026: KIUT Stands for Equality

International Women’s Day 2026: KIUT Stands for Equality

Mar 19, 2026

MAMODEX Advances to Operational Phase of Project

MAMODEX Advances to Operational Phase of Project

Mar 20, 2026